Jumatano, 10 Agosti 2016

ITV,CLOUDS TV NA CLOUDS REDIO VYAPIGWA FAINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipatia onyo na kuvipiga faini ya shiilingi milioni 19 vituo vya ITV na Clouds TV pamoja na  kimoja cha redio ambacho ni Clouds Fm kwa kosa la kukiuka maadili ya utangazaji.
Akitoa uamuzi huo uliofikiwa na Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema kwamba vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni na taratibu za Huduma ya Utangazaji na kuvitaka kuwa wawe wasimamizi wazuri wa vipindi vyao.

Mapunda aliendelea kwa kusema kamati hiyo imekipa onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10 kituo cha televisheni cha ITV kwa makosa mawili,kosa  la kwanza ni kupitia kipindi chake cha Kumekucha cha Juni 15, mwaka huu kilichoruka hewani kati ya saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambacho mtangazaji alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuhusiana na  mwenendo wa Bunge la Bajeti, lakini Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson lakini mtangazaji hakuchukua hatua zozote za kumuomba Mheshimiwa Msigwa kufuta lugha ya matusi alioitumia.
Na kosa la pili,  kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari ya Juni 23 kati ya saa 1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa miaka 16 aliyebakwa na kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana huyo kwa jina na shule anayosoma.Na katika utetezi wake mwakilishi kutoka ITV,Steven Chuwa alikiri kuwa Mchungaji Msigwa alitoa maneno ya kashfa na hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.

Aidha alisema kama mtangazaji angemuomba kufuta kauli, mjadala ungekuwa mkubwa zaidi Alisema watachukua hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.Kwa upande wa Kituo cha Clouds Tv, kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni nne ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.

Mapunda alisema kituo hicho kupitia kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya saa 8:00 mchana na 12:00 jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja wa Mwana FA na Break It Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa mwanamke.

Vile vile,Clouds Fm pia imepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi vyake vya ‘Power Breakfast’ na Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.Na katika kipindi cha Jahazi cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55 jioni, watangazaji walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na mbuzi, ambako walieleza kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake, jambo lililoonesha wanahamasisha vitendo hivyo.

Aidha, Mei 18, mwaka huu katika kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa 12:00 na 4:00 asubuhi baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu kupandikizwa kwa sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu, aliyezaliwa akiwa hana na kulelewa kama mtoto wa kike.

Jumamosi, 16 Julai 2016

BASATA KUUFUNGIA WIMBO WA PALE KATI WA MSANII NEY WA MITEGO




Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania  (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa msanii Ney wa mitego uitwao Pale kati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye kukiuka maadili.

Alisema“Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.'

Aidha aliongeza kwa kusema wao BASATA waliwahi kumuita msanii huyo mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama

RAISI MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE

Leo tarehe 16 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli  amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1)Augustino Lyatonga Mrema.
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
⦁ Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
2)Prof. William R. Mahalu
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
3Prof. Mohamed Janabi
⦁ Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
4)Prof. Angelo Mtitu Mapunda
⦁ Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
 5)Sengiro Mulebya
⦁ Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
6)Oliva Joseph Mhaiki
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
7)Winifrida Gaspar Rutaindurwa
⦁ Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
8)Charles Rukiko Majinge
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
9)Dkt. Julius David Mwaiselage
⦁ Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Hali kadhalika Rais  Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1)Essaka Ndege Mugasa
2)Adamson Afwilile Mponi
3)Charles Ndalahwa Julius Kenyela
4)Richard Malika Revocatus
5)Geofrey Yesaya Kamwela
6)Lucas John Mkondya
7)John Mondoka Gudaba
8)Matanga Renatus Mbushi
9)Frasser Rweyemamu Kashai
10)Ferdinand Elias Mtui
11)Germanus Yotham Muhume
12)Fulgence Clemence Ngonyani
13)Modestus Gasper Lyimo
14)Mboje John Shadrack Kanga
15)Gabriel G.A. Njau
16)Ahmed Zahor Msangi
17)Anthony Jonas Rutashubulugukwa
18)Dhahir Athuman Kidavashari
19)Ndalo Nicholus Shihango
20)Shaaban Mrai Hiki
21)Simon Thomas Chillery
22)Leonard Lwabuzara Paul
23)Ahmada Abdalla Khamis
24)Aziz Juma Mohamed
25)Juma Yussuf Ally

Vilevile, Rais  John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)kuanzia july 15 mwaka huu.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1)Fortunatus Media Musilimu
2)Goyayi Mabula Goyayi
3)Gabriel Joseph Mukungu
4)Ally Omary Ally
5)Edward Selestine Bukombe
6)Sifael Anase Mkonyi
7)Naftari J. Mantamba
8)Onesmo Manase Lyanga
9)Paul Tresphory Kasabago
10)Dadid Mshahara Hiza
11)Robert Mayala
12)Lazaro Benedict Mambosasa
13)Camilius M. Wambura
14)Mihayo Kagoro Msikhela
15)Ramadhani Athumani Mungi
16)Henry Mwaibambe Sikoki
17)Renata Michael Mzinga
18)Suzan Salome Kaganda
19)Neema M. Mwanga
20)Mponjoli Lotson
21)Benedict Michael Wakulyamba
22)Wilbroad William Mtafungwa
23)Gemini Sebastian Mushi
24)Peter Charles Kakamba
25)Ramadhan Ng’anzi Hassan
26)Christopher Cyprian Fuime
27)Charles Philip Ulaya
28)Gilles Bilabaye Muroto
29)Mwamini Marco Lwantale
30)Allute Yusufu Makita
31)Kheriyangu Mgeni Khamis
32)Nassor Ali Mohammed 
33)Salehe Mohamed Salehe
34)Mohamed Sheikhan Mohamed

Jumanne, 12 Julai 2016

RAISI MAGUFULI AAGIZA VYOMBO VYA SERIKALI KUTUMIA MASHINE ZA EFD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
 
“Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani  wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.
 
Aidha amewataka wakurugenzi  wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
 
Hali kadhalika amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana  na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
  .
 
Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.


ETHIOPIA YAZIMA MITANDAO YA KIJAMII

Waethiopia waliamka Wikiendi wakajikuta hawana huduma hizo za mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber ambapo Serikali imefunga mitandao hiyo tangu Jumamosi usiku.

Msemaji wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa serikali ilichukua hatua hiyo kama njia ya kuzuia wanafunzi wasivurugwe na ushawishi wa mitandao hiyo ya kijami na hatua hiyo imetokea majuma kadhaa baada ya baadhi ya makaratasi ya mitihani kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimu serikali kufutilia mbali mitihani hiyo iliyodukuliwa.''Serikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano.

Tumegundua kuwa mitandao ya kijamii huvuruga kabisa ratiba ya vijana na haswa wanafunzi'', alisema msemaji wa serikali Getachew RedaSerikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano mitihani itakapokuwa imekamilika

Hatu hiyo  ya kuifungia mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na Instagram bila shaka imewaudhi wanaharakati wa kupigania uhuru wa habari nchini Ethiopia.

DKT MWAKA KUFUTIWA USAJILI WAKE

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na  Dokta  Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.



Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Vilevile amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.Na Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai.

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.

Jumapili, 10 Julai 2016

WAKURUGENZI WAPYA WALIOCHAGULIWA WATAKIWA KUKAGULIWA VYETI KABLA YA KUAPISHWA

Wakurugenzi wa halmashauri za majiji 21, manispaa 5, miji 22 na wilaya 137 nchi nzima   walioteuliwa Jumatano ya wiki hii, wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapishwa keshokutwa ikulu jijini dar es salaam.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari, imewataka wakurugenzi hao kuwa watakapofika kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma, wahakikishe wanafika na nakala zao halisi za vyeti vya kitaaluma kwa ajili ya ukaguzi.

“Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli,” imeeleza taarifa hiyo iliyotumwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

Aidha taarifa hiyo iliendelea kwa  kusema kuwa uhakiki huo wa vyeti utaanza saa mbili asubuhi na kuwataka wahusika wote kuingia Ikulu kwa kupitia geti kuu lililopo upande wa Mashariki, linalotazamana na bahari ya Hindi. ..

Uhakiki wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika mwaka huo, ulibaini kuwa baadhi ya watumishi wakiwemo wa serikali walikuwa  wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo vimebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vya bandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.

Mwaka huo huo, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ilitoa taarifa ikieleza kubaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012; watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.

Kutokana na hali hiyo, Necta ilitangaza kuanza kujipanga kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa kwani lilishakuwa tatizo kubwa nchini Tanzania.

Ijumaa, 8 Julai 2016

RAISI MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE




Taarifa kutoka ikulu nchini Tanzania ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli amemteua Dk. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza July 07 2016. Kabla ya uteuzi huu Dk. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).

 Dk. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu June 30 mwaka huu

Alhamisi, 7 Julai 2016

IKULU YATOA TAARIFA YA MAREKEBISHO

Taarifa kutokea Ikulu nchini Tanzania, inasema kwamba kuna marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya iliyotolewa hapo awali ambapo Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Taarifa hiyo inasema kwamba Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa  hapo baadaye.

Jumatano, 6 Julai 2016

MOURINHO AMSAJILI STAA MPYA

Kocha mpya wa klabu ya manchester united Jose Mourinho amemsajili staa mpya leo tarehe 6,Henrikh Mkhitaryan kutokea klabu ya Borussia  Dortmund kwa mkataba wa miaka mine.




Mkhitaryan anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Man United baada ya kusajiliwa kwa Eric Bailly kutoka  Villarreal na Zlatan Ibrahimovic kama
mchezaji huru.

Jumanne, 5 Julai 2016

EID ULL FITRI KUADHIMISHWA KESHO

Sikukuu ya Eid Mubarak kuadhimishwa kesho baada ya kiashiria kinachoaminiwa kuwa kikionekana bhasi ndio sikukuu yenyewe inaadhimishwa kuonekana.maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania .
Uthibitisho umetolewa na Mufti mkuu wa Tanzania Zubeir Bin Ally leo  kuwa kesho ndio sikuu ya Eid Ull Fitri

TFDA YATOA RAI KWA JAMII IWE INATOA TAAARIFA JUU YA MATUMIZI YA DAWA

   Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA),imetoa rai kwa wataalam wa afya na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa juu ya madhara yoyote yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kutumia mfumo mpya wa kieletroniki unaotumia computer na smartphone.
   Hayo yamesemwa na meneja mawasiliano wa mamlaka hiyo bi Gaudensia Mwisenza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mazima ya utoaji taarifa na kufafanua zaidi majukumu yao.
  Aidha Afisa wa kitengo cha usalama wa majaribio ya dawa katika mamlaka hiyo Dr Alex Kayamba alielza jinsi ya kutumia mfumo huo wa kieletroniki kwa kuingia internet na kwa wale ambao hawana smart phone wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kufanya ili nao waweze kutoa taarifa kama wengine kwani kwa sasa mfumo huo upo kwenye majaribio na haujazinduliwa rasmi kabisa.

Jumatatu, 4 Julai 2016

Taasisi ya maridhiano Tanzania ambayo inaundwa na madhehebu ya dini tofauti tofauti nchini,imejitambulisha rasmi kwa jamii pamoja na kueleza kazi zao wanazozifanya katika taasisi hiyo.
Aidha taasisi hiyo itafanya shughuli ya uzinduzi wa taasisi hiyo siku ya 13/07/2016 katika ukumbi wa Karimjee jijini dar es salaam,kuanzia saa kumi jioni hadi saa moja na nusu jioni na mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakua waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Vilevile shughuli hizo zitaambatana na utoaji wa Tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamechangia kudumisha amani na watu hao ni kama wafuatao:Mama Maria Nyerere,Jakaya Mrisho Kikwete,IGP Saidi Mwema,Reginald Mengi,Mustafa Sabodo,Helen Simba,Sadick Meck Sadick,Ruge Mutahaba,Albert Sanga(mwanzilishi wa bunge la uchumi nchini).

Alhamisi, 30 Juni 2016

SIMBA SPORTS CLUB IMETHIBITISHA KUHUSU KOCHA MKUU WA TIMU HIYO


Klabu ya Simba Fc Imethibitisha rasmi kuwa mkameroon Joseph Omog kuwa ndiye kocha kuu wa timu hiyo.Lakini pia kocha huyo aliwah isaidia Azam Fc kupata ubingwa msimu wa 2013/2014.






Jumanne, 28 Juni 2016

TP MAZEMBE YAIKONG’OLI YANGA KAMOJA UWANJA WA TAIFA

index 
Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Obrey Chirwa akiichambua ngome ya timu ya TP Mazembe, katika mtanange uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam, ikiwa ni Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hadi kupanga cha mwisho kinalia, Yanga wamelala kwa bao 1-0.(Picha na michuziblog)
tai2  
Mashabiki wakiwa wamefurikwa kwenye uwanja wa Taifa hata hivyo mwishowe wakaondoka vichwa chini baada ya timu yao kupoteza mchezo huo mbele ya mahasimu wao TP Mazembe

SHAMO WORLD YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.

 Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu vya msaada kwa  Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif jijini Dar  es Salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika  kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.
 
Nae Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
 
Mwakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg 50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia.
 Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama  na Zaituni Ramadhani wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na watoto walio klatika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.

WIZARA YA ARDHI YAANZA KUTOA HUDUMA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

MAB1 
Banda la maonesho la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi likiwa limeanza rasmi kutoa huduma katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere vya Sabasaba Dar es salaam.
MAB2 
Baadhi ya Wananchi wakipata maelezo ya huduma za mipango miji zinazosimamiwa na Wizara ya Ardhi.
MAB3 Muoneshaji wa Wizara ya Ardhi bi. Mwanamkuu Ally akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Ardhi kifaa kinachotumika katika upimaji wa Ardhi cha aina ya Total station.

Tatizo la mikopo kupatiwa ufumbuzi

TANT1 
Wananchi mbalimbali wakiingia katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa kwa ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali.Maonyesho hayo yameanza leo hii Jijini Dar es salaam.Picha n Daudi Manongi,MAELEZO
TANT01 
Askari wa JKT pamoja na FFU wakihakikisha usalama wakati wananchi wakiingia katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuangalia bidhaa mbalimbali baada  ya maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa kuanza leo jijini Dar es salaam.
TANT3 
Afisa Habari Idara ya Habari,MAELEZO Bi.Immaculate Makilika akizungumza jambo na Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Bw.Baruti Mwaigaga(kushoto)  katika banda la Wizara hiyo viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
TANT4Mwananchi akiangalia moja ya bidhaa  zinazotengenezwa na kikundi cha African Flowerless fashion cha Arusha kinachouza bidhaa zake nje ya nchi.Kulia ni Afisa wa kikundi hicho Bi.Suzana Mwalongo.
TANT5 
Mafundi wakiendelea na upakaji rangi katika banda la CRDB katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar e Salaam.
…………………………………………………………………………………
Na: Immaculate Makilika- MAELEZO, Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja vya  Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.
“Kufuatia kuwepo kwa tatizo kubwa la upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda hapa nchini, Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa taarifa zinazohusu upatikanaji wa mikopo ili kusaidia wananchi, kitu ambacho hakikuwepo awali” alisema Bw. Mwaigaga
Alisema lengo la mkakati huo ni kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha kiwanda kupata taarifa sahihi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kupata mkopo ambao unaondoa usumbufu kwa walengwa ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mikakati mingine ya Serikali katika kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na kuanzisha programu ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya Ruvuma, Pwani, Iringa, Tanga na Manyara.
Naye, Afisa Uchumi kutoka Wizara hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Wizara inawaunganisha wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na kuwapatia masoko ya mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya Oramu pamoja na Murza Mills.
Aidha, wananchi wamesisitizwa kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara  pamoja na taasisi zake za BRELA, TBS, TFDA , CBE na SIDO lililopo katika viwanja hivyo vya maonesho ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu namna za kufanya biashara pamoja na kuanzisha viwanda nchini.

LESOTHO YAKUBALI KUTEKELEZA MASHARTI YA SADC

NAM1 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki akatika Mkutano wa  Viongozi  Wakuu wa  Nchi  na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC) uliofanyika kwenye hoteli ya Grand Palm  mjini Gaborone Botswana Juni 28. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili amekubali kutekeleza masharti yaliyowekwa na Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), na kuridhia timu ya uchunguzi kwenda nchini humo kufanya uchunguzi wa hali ya kiusalama na kisiasa.
Dk. Mosisili ametoa uamuzi huo leo (Jumanne, 28 Juni, 2016) wakati wa kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.
Pia amekubali viongozi waupinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko yaliyotokea nchini humo warejee nchini mwao na kuahidi kwamba atahakikisha wanapatiwa ulinziwa kutosha.
Januari mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagizakwambaifikapo Februari Mosi, mwaka huuSerikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa na kiusalama nchini humo hususan mazingira yaliyopelekea kifo cha marehemu Luteni Jenerali Maaparankoe Mahao ambaye alikuwa Mkuuwa Majeshi.
Kwaupande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kikao hicho amesema wamepitia ripoti iliyoundwa na timu ya SADC iliyochunguza kuhusu matatizo ya Lethoto ambayo iliwahoji Viongozi wa Serikali, Jeshi, Bunge na familia ya marehemu Luteni Jenerali Mahao.
“Lengo la hatuahiiza SADC ni kuhakikisha inarejesha hali ya amani na utulivu kwenye maeneo ya siasa, ulinzi na usalama katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili wananchi wake waweze kuishi vizuri,” amesema
Pia Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Wakuu wa Nchina Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika Summit), Agosti mwaka huu ambapo kitafanyika kikao kingine nchini  Tanzania.
Mkutano huo wa ulifunguliwa na Rais wa Botswana, Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama na ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli;  Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Rais wa Zimbabwe, Bw. Robert Mugabe, Mfalme Muswati wa III wa Swazland.
SADC Double Troika ni kikao maalum kinachojumuisha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation). 
SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.
Chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).
Wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaunda SADC Summit.

TAARIFA YA UTEUZI KWA VYOMBO VYA HABARI

index 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).  Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9 (1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya kufanya uteuzi huo.  Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt. Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri – Sanaa (M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.
Imetolewa na,
Genofeva Matemu,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
28 Juni,2016

Jumamosi, 25 Juni 2016

MR NICE ATOA ALBAM YAKE MPYA


WhatsApp-Image-20160624 (1)












   Msanii wa muziki nchini Mr nice ameachia ablam yake iitwayo KIOO siku ya jumatano huko nchini Kenya na mauzo yake kuwa makubwa kufikia nakala 5000.
Msanii huyo amesema kuwa kama alivyoahidi kutoa albamu tu na sio single tena kwani natembea kiutu uzima,na mpaka sasa ameuza nakala hizo 5000 katika nchi ya kenya tu hivyo bado nchi zingine pia.
   Mr Nice kwa sasa yupo nchini Kenya kwa ajili ya kuitangaza albamu yake mpya huku akifanya show mbalimbali na anategemea akimaliza nchini hapo ataelekea nchini Uganada.

SHILOLE AFUNGUA LABEL YAKE NA KUMSAINI MSANII CHIPUKIZI


11330616_296972493806688_1211325526_n
         Zuwena Mohamed "Shilole"

   Msanii wa muziki nchini Zuwena Mohamed almaarufu kwa jina la Shilole,ameanzisha label yake iitwayo Shilole Entertaiment,lakini pia kumsaini msanii chipukizi aitwae Amaselly.

   Shilole amefunguka kwa kusema ameamua kuanzisha label hiyo ili kuwasaidia wasanii ambao wana vipaji ila hawapati nafasi kwenye game
      Kwa upande wake msanii huyo Amaseiil a.k.a Gaucho,amesema kuwa alimshukuru shilole kwa uamuzi huo wa kumsainisha kwenye label yake hivyo anaahidi mambo mazuri katika game ya muziki.

Alhamisi, 23 Juni 2016

YANGA YATOA TAMKO KUHUSIANA NA MECHI YAO NA TP MAZEMBE


http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/06/IMG-20160623-WA0011.jpg

MASHINDANO YA KUSOMA QURAAN YA KIMATAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO USIKU

   Jumuiya ya kuhifadhisha Quraan Tanzania imetangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya kusoma Quraan ya kimataifa kuanzia leo usiku baada ya swala ya Tarawee katika msikiti wa mtoro jijini dar es salaam na kilele chake kuwa ni siku ya jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
   Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Shekhe Otham Ally Katoro wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa na kutoa ufafanuzi wa mashindano hayo kwa ujumla wake.
   Aidha Shekhe Othman alisema kuwa kila nchi imetoa mshiriki mmoja na wote wamekariri juzuu zote thelathini za kitabu cha Quraan na washindikatika shindano hilo watazawaida pesa kuanzia dola 5000.
    Mashindano hayo yana jumla ya washiriki 22 na yataanza leo na kuendelea hadi siku ya jumapili  ambayo ndio kilele chake katika ukumbi wa Diamond Jubilee na mgeni rasmi siku hiyo ni waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Jumatano, 22 Juni 2016

KUPATWA KWA JUA KIPETE KUNATARAJIA KUTOKEA TANZANIA

Chuo kikuu huria nchini Tanzania,kimetangaza tukio la kupatwa kwa jua kipete ambalo linatarajia kutokea septemba mosi mwaka huu,hivyo macho yote yataelekezwa nchini Tanzania ili kushuhudia tukio hilo.
Hayo yamezungumzwa na Dk Nooraj T Jiwaji ambaye ni mtaalam wa kitivo cha sayansi na teknolojia na elimu ya mazingira katika chuo hiko wakati akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam.
Tukio ilo ambalo ni nadra sana kutokea hasa kwa kizazi hiki cha sasa ambalo huwa linatokea kila baada ya miaka 15,hivyo linatarajiwa kutokea septemba mosi na hivyo wananchi na jamii nzima kwa ujumla wataelekea Rujewa karibu kabisa na mkoa wa Mbeya,kusini mwa Tanzania kushuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua.