Jumamosi, 16 Julai 2016

BASATA KUUFUNGIA WIMBO WA PALE KATI WA MSANII NEY WA MITEGO




Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania  (BASATA) limeufungia rasmi wimbo wa msanii Ney wa mitego uitwao Pale kati kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili ya kitanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa msanii huyo amekuwa na tabia na mienendo yenye kuchafua sekta ya sanaa yeye binafsi kupitia kutoa kazi chafu na kufanya maonyesho yenye kukiuka maadili.

Alisema“Kazi zake zikikiuka maadili na kudhalilisha utu wa mwanamke sambamba na kutoa lugha za matusi na za kudhalilisha watu wa kada mbalimbali.'

Aidha aliongeza kwa kusema wao BASATA waliwahi kumuita msanii huyo mara kadhaa kutokana na tabia yake ya kutoa kazi zisizokuwa na maadili na aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio haya kwa makusudi ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu kazi ya sanaa kama kazi nyingine. Kwa sasa Msanii huyu ametoa wimbo mwingine wa ambao uko mitandaoni ukipambwa na picha chafu zinazoonesha mwanamke akiwa mtupu yaani uchi wa mnyama

RAISI MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE

Leo tarehe 16 mwaka 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli  amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1)Augustino Lyatonga Mrema.
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
⦁ Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
2)Prof. William R. Mahalu
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
3Prof. Mohamed Janabi
⦁ Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
4)Prof. Angelo Mtitu Mapunda
⦁ Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
 5)Sengiro Mulebya
⦁ Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
6)Oliva Joseph Mhaiki
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
7)Winifrida Gaspar Rutaindurwa
⦁ Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
8)Charles Rukiko Majinge
⦁ Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
9)Dkt. Julius David Mwaiselage
⦁ Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Hali kadhalika Rais  Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1)Essaka Ndege Mugasa
2)Adamson Afwilile Mponi
3)Charles Ndalahwa Julius Kenyela
4)Richard Malika Revocatus
5)Geofrey Yesaya Kamwela
6)Lucas John Mkondya
7)John Mondoka Gudaba
8)Matanga Renatus Mbushi
9)Frasser Rweyemamu Kashai
10)Ferdinand Elias Mtui
11)Germanus Yotham Muhume
12)Fulgence Clemence Ngonyani
13)Modestus Gasper Lyimo
14)Mboje John Shadrack Kanga
15)Gabriel G.A. Njau
16)Ahmed Zahor Msangi
17)Anthony Jonas Rutashubulugukwa
18)Dhahir Athuman Kidavashari
19)Ndalo Nicholus Shihango
20)Shaaban Mrai Hiki
21)Simon Thomas Chillery
22)Leonard Lwabuzara Paul
23)Ahmada Abdalla Khamis
24)Aziz Juma Mohamed
25)Juma Yussuf Ally

Vilevile, Rais  John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)kuanzia july 15 mwaka huu.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1)Fortunatus Media Musilimu
2)Goyayi Mabula Goyayi
3)Gabriel Joseph Mukungu
4)Ally Omary Ally
5)Edward Selestine Bukombe
6)Sifael Anase Mkonyi
7)Naftari J. Mantamba
8)Onesmo Manase Lyanga
9)Paul Tresphory Kasabago
10)Dadid Mshahara Hiza
11)Robert Mayala
12)Lazaro Benedict Mambosasa
13)Camilius M. Wambura
14)Mihayo Kagoro Msikhela
15)Ramadhani Athumani Mungi
16)Henry Mwaibambe Sikoki
17)Renata Michael Mzinga
18)Suzan Salome Kaganda
19)Neema M. Mwanga
20)Mponjoli Lotson
21)Benedict Michael Wakulyamba
22)Wilbroad William Mtafungwa
23)Gemini Sebastian Mushi
24)Peter Charles Kakamba
25)Ramadhan Ng’anzi Hassan
26)Christopher Cyprian Fuime
27)Charles Philip Ulaya
28)Gilles Bilabaye Muroto
29)Mwamini Marco Lwantale
30)Allute Yusufu Makita
31)Kheriyangu Mgeni Khamis
32)Nassor Ali Mohammed 
33)Salehe Mohamed Salehe
34)Mohamed Sheikhan Mohamed

Jumanne, 12 Julai 2016

RAISI MAGUFULI AAGIZA VYOMBO VYA SERIKALI KUTUMIA MASHINE ZA EFD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
 
“Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani  wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.
 
Aidha amewataka wakurugenzi  wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
 
Hali kadhalika amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana  na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
  .
 
Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.


ETHIOPIA YAZIMA MITANDAO YA KIJAMII

Waethiopia waliamka Wikiendi wakajikuta hawana huduma hizo za mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber ambapo Serikali imefunga mitandao hiyo tangu Jumamosi usiku.

Msemaji wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa serikali ilichukua hatua hiyo kama njia ya kuzuia wanafunzi wasivurugwe na ushawishi wa mitandao hiyo ya kijami na hatua hiyo imetokea majuma kadhaa baada ya baadhi ya makaratasi ya mitihani kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimu serikali kufutilia mbali mitihani hiyo iliyodukuliwa.''Serikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano.

Tumegundua kuwa mitandao ya kijamii huvuruga kabisa ratiba ya vijana na haswa wanafunzi'', alisema msemaji wa serikali Getachew RedaSerikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano mitihani itakapokuwa imekamilika

Hatu hiyo  ya kuifungia mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na Instagram bila shaka imewaudhi wanaharakati wa kupigania uhuru wa habari nchini Ethiopia.

DKT MWAKA KUFUTIWA USAJILI WAKE

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na  Dokta  Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.



Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Vilevile amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya hivyo.Na Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai.

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.

Jumapili, 10 Julai 2016

WAKURUGENZI WAPYA WALIOCHAGULIWA WATAKIWA KUKAGULIWA VYETI KABLA YA KUAPISHWA

Wakurugenzi wa halmashauri za majiji 21, manispaa 5, miji 22 na wilaya 137 nchi nzima   walioteuliwa Jumatano ya wiki hii, wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapishwa keshokutwa ikulu jijini dar es salaam.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari, imewataka wakurugenzi hao kuwa watakapofika kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma, wahakikishe wanafika na nakala zao halisi za vyeti vya kitaaluma kwa ajili ya ukaguzi.

“Ieleweke kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli,” imeeleza taarifa hiyo iliyotumwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa.

Aidha taarifa hiyo iliendelea kwa  kusema kuwa uhakiki huo wa vyeti utaanza saa mbili asubuhi na kuwataka wahusika wote kuingia Ikulu kwa kupitia geti kuu lililopo upande wa Mashariki, linalotazamana na bahari ya Hindi. ..

Uhakiki wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) katika mwaka huo, ulibaini kuwa baadhi ya watumishi wakiwemo wa serikali walikuwa  wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo vimebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vya bandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.

Mwaka huo huo, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, ilitoa taarifa ikieleza kubaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012; watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.

Kutokana na hali hiyo, Necta ilitangaza kuanza kujipanga kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa kwani lilishakuwa tatizo kubwa nchini Tanzania.

Ijumaa, 8 Julai 2016

RAISI MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE




Taarifa kutoka ikulu nchini Tanzania ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli amemteua Dk. Leonard Lutegama Maboko kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS).

Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza July 07 2016. Kabla ya uteuzi huu Dk. Leonard Lutegama Maboko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu Mbeya (NIMR Mbeya).

 Dk. Leonard Lutegama Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Fatma Mrisho ambaye mkataba wake umemalizika tangu June 30 mwaka huu

Alhamisi, 7 Julai 2016

IKULU YATOA TAARIFA YA MAREKEBISHO

Taarifa kutokea Ikulu nchini Tanzania, inasema kwamba kuna marekebisho madogo katika majina yaliyopo kwenye orodha ya wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya iliyotolewa hapo awali ambapo Dkt. Leonard Moses Massale ametangazwa kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma.

Taarifa hiyo inasema kwamba Jina hilo limeingizwa katika Orodha ya Wakurugenzi wa halmashauri kwa makosa na kwa sababu hiyo Dkt. Leonard Moses Massale anaendelea kuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza. Kufuatia marekebisho hayo, uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma utatangazwa  hapo baadaye.

Jumatano, 6 Julai 2016

MOURINHO AMSAJILI STAA MPYA

Kocha mpya wa klabu ya manchester united Jose Mourinho amemsajili staa mpya leo tarehe 6,Henrikh Mkhitaryan kutokea klabu ya Borussia  Dortmund kwa mkataba wa miaka mine.




Mkhitaryan anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Man United baada ya kusajiliwa kwa Eric Bailly kutoka  Villarreal na Zlatan Ibrahimovic kama
mchezaji huru.

Jumanne, 5 Julai 2016

EID ULL FITRI KUADHIMISHWA KESHO

Sikukuu ya Eid Mubarak kuadhimishwa kesho baada ya kiashiria kinachoaminiwa kuwa kikionekana bhasi ndio sikukuu yenyewe inaadhimishwa kuonekana.maeneo mbalimbali ya nchini Tanzania .
Uthibitisho umetolewa na Mufti mkuu wa Tanzania Zubeir Bin Ally leo  kuwa kesho ndio sikuu ya Eid Ull Fitri

TFDA YATOA RAI KWA JAMII IWE INATOA TAAARIFA JUU YA MATUMIZI YA DAWA

   Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA),imetoa rai kwa wataalam wa afya na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa juu ya madhara yoyote yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kutumia mfumo mpya wa kieletroniki unaotumia computer na smartphone.
   Hayo yamesemwa na meneja mawasiliano wa mamlaka hiyo bi Gaudensia Mwisenza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mazima ya utoaji taarifa na kufafanua zaidi majukumu yao.
  Aidha Afisa wa kitengo cha usalama wa majaribio ya dawa katika mamlaka hiyo Dr Alex Kayamba alielza jinsi ya kutumia mfumo huo wa kieletroniki kwa kuingia internet na kwa wale ambao hawana smart phone wanaangalia ni jinsi gani wanaweza kufanya ili nao waweze kutoa taarifa kama wengine kwani kwa sasa mfumo huo upo kwenye majaribio na haujazinduliwa rasmi kabisa.

Jumatatu, 4 Julai 2016

Taasisi ya maridhiano Tanzania ambayo inaundwa na madhehebu ya dini tofauti tofauti nchini,imejitambulisha rasmi kwa jamii pamoja na kueleza kazi zao wanazozifanya katika taasisi hiyo.
Aidha taasisi hiyo itafanya shughuli ya uzinduzi wa taasisi hiyo siku ya 13/07/2016 katika ukumbi wa Karimjee jijini dar es salaam,kuanzia saa kumi jioni hadi saa moja na nusu jioni na mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakua waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Vilevile shughuli hizo zitaambatana na utoaji wa Tuzo kwa watu mbalimbali ambao wamechangia kudumisha amani na watu hao ni kama wafuatao:Mama Maria Nyerere,Jakaya Mrisho Kikwete,IGP Saidi Mwema,Reginald Mengi,Mustafa Sabodo,Helen Simba,Sadick Meck Sadick,Ruge Mutahaba,Albert Sanga(mwanzilishi wa bunge la uchumi nchini).