Jumatano, 10 Agosti 2016

ITV,CLOUDS TV NA CLOUDS REDIO VYAPIGWA FAINI

Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipatia onyo na kuvipiga faini ya shiilingi milioni 19 vituo vya ITV na Clouds TV pamoja na  kimoja cha redio ambacho ni Clouds Fm kwa kosa la kukiuka maadili ya utangazaji.
Akitoa uamuzi huo uliofikiwa na Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mapunda alisema kwamba vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni na taratibu za Huduma ya Utangazaji na kuvitaka kuwa wawe wasimamizi wazuri wa vipindi vyao.

Mapunda aliendelea kwa kusema kamati hiyo imekipa onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10 kituo cha televisheni cha ITV kwa makosa mawili,kosa  la kwanza ni kupitia kipindi chake cha Kumekucha cha Juni 15, mwaka huu kilichoruka hewani kati ya saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambacho mtangazaji alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kuhusiana na  mwenendo wa Bunge la Bajeti, lakini Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson lakini mtangazaji hakuchukua hatua zozote za kumuomba Mheshimiwa Msigwa kufuta lugha ya matusi alioitumia.
Na kosa la pili,  kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari ya Juni 23 kati ya saa 1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa miaka 16 aliyebakwa na kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana huyo kwa jina na shule anayosoma.Na katika utetezi wake mwakilishi kutoka ITV,Steven Chuwa alikiri kuwa Mchungaji Msigwa alitoa maneno ya kashfa na hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.

Aidha alisema kama mtangazaji angemuomba kufuta kauli, mjadala ungekuwa mkubwa zaidi Alisema watachukua hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.Kwa upande wa Kituo cha Clouds Tv, kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni nne ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.

Mapunda alisema kituo hicho kupitia kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya saa 8:00 mchana na 12:00 jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja wa Mwana FA na Break It Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa mwanamke.

Vile vile,Clouds Fm pia imepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi vyake vya ‘Power Breakfast’ na Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.Na katika kipindi cha Jahazi cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55 jioni, watangazaji walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na mbuzi, ambako walieleza kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake, jambo lililoonesha wanahamasisha vitendo hivyo.

Aidha, Mei 18, mwaka huu katika kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa 12:00 na 4:00 asubuhi baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhusu kupandikizwa kwa sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu, aliyezaliwa akiwa hana na kulelewa kama mtoto wa kike.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni