Alhamisi, 23 Juni 2016

MASHINDANO YA KUSOMA QURAAN YA KIMATAIFA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEO USIKU

   Jumuiya ya kuhifadhisha Quraan Tanzania imetangaza rasmi kuanza kwa mashindano ya kusoma Quraan ya kimataifa kuanzia leo usiku baada ya swala ya Tarawee katika msikiti wa mtoro jijini dar es salaam na kilele chake kuwa ni siku ya jumapili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
   Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Shekhe Otham Ally Katoro wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa na kutoa ufafanuzi wa mashindano hayo kwa ujumla wake.
   Aidha Shekhe Othman alisema kuwa kila nchi imetoa mshiriki mmoja na wote wamekariri juzuu zote thelathini za kitabu cha Quraan na washindikatika shindano hilo watazawaida pesa kuanzia dola 5000.
    Mashindano hayo yana jumla ya washiriki 22 na yataanza leo na kuendelea hadi siku ya jumapili  ambayo ndio kilele chake katika ukumbi wa Diamond Jubilee na mgeni rasmi siku hiyo ni waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni