Tatizo la mikopo kupatiwa ufumbuzi
Wananchi
mbalimbali wakiingia katika Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa kwa
ajili ya kujipatia bidhaa mbalimbali.Maonyesho hayo yameanza leo hii
Jijini Dar es salaam.Picha n Daudi Manongi,MAELEZO
Askari
wa JKT pamoja na FFU wakihakikisha usalama wakati wananchi wakiingia
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kuangalia bidhaa mbalimbali baada ya
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa kuanza leo jijini Dar es
salaam.
Afisa
Habari Idara ya Habari,MAELEZO Bi.Immaculate Makilika akizungumza jambo
na Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji
Bw.Baruti Mwaigaga(kushoto) katika banda la Wizara hiyo viwanja vya
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mafundi
wakiendelea na upakaji rangi katika banda la CRDB katika Maonyesho ya
40 ya Biashara ya Kimataifa viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar e
Salaam.
…………………………………………………………………………………
Na: Immaculate Makilika- MAELEZO, Dar es salaam.
SERIKALI kupitia Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi
tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini
ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.
Hayo yamesemwa na Afisa Biashara
wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja
vya Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza leo jijini
Dar es Salaam.
“Kufuatia kuwepo kwa tatizo
kubwa la upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye nia ya kuanzisha viwanda
hapa nchini, Serikali imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa taarifa
zinazohusu upatikanaji wa mikopo ili kusaidia wananchi, kitu ambacho
hakikuwepo awali” alisema Bw. Mwaigaga
Alisema lengo la mkakati huo
ni kumrahisishia mwananchi mwenye nia ya kuanzisha kiwanda kupata
taarifa sahihi ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kupata mkopo ambao
unaondoa usumbufu kwa walengwa ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali
ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Mikakati mingine ya Serikali
katika kukuza sekta ya viwanda nchini ni pamoja na kuanzisha programu ya
kuendeleza viwanda vidogo vidogo katika mikoa ya Ruvuma, Pwani, Iringa,
Tanga na Manyara.
Naye, Afisa Uchumi kutoka Wizara
hiyo Bw. Vicent Turuka alisema katika kutekeleza azma ya Serikali ya
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, Wizara inawaunganisha
wafanyabiasha wadogo wadogo na wanunuzi wakuu na kuwapatia masoko ya
mazao mfano zao la ufuta lina soko kwa kampuni ya Oramu pamoja na Murza
Mills.
Aidha, wananchi wamesisitizwa
kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Bishara pamoja na taasisi zake
za BRELA, TBS, TFDA , CBE na SIDO lililopo katika viwanja hivyo vya
maonesho ili kupata taarifa mbalimbali kuhusu namna za kufanya biashara
pamoja na kuanzisha viwanda nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni