SHAMO WORLD YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA JIJINI DAR LEO.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Shamo World Foundtion, Salama akikabidhi baadhi ya Vitu
vya msaada kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga
Centre, Zainabu Maunga jijini Dar es Salaam leo wakati walipotembelea
katika kituo hicho kilichopo karibu na kituo cha Polisi cha Hananasif
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo mwakilishi wa kampuni ya Shamo World
Foundation amesema kuwa wameguswa kutoa msaada katika kituo hicho kwa
kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki cha Mwezi wa Ramadhani
kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia ugumu wa
maisha walezi wa watoto hao.
Nae Mlezi
Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre, Zainabu
Maunga amewashukuru kampuni ya Shamo World kuwaona kwa jicho la pekee na
kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama amesema kampuni hiyo
wamekabidhi Kg 50 za Mchele, Kg 50 za unga wa ngano na unga wa ugali, Kg
50 za sukari pamoja na Maboksi 15 ya Tende pamoja na mafuta ya kupikia.
Wawakilishi
wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama na Zaituni Ramadhani
wakikabidhi mafuta ya kupikia kwa watoto kwa kituo cha kulelea watoto
yatima cha Maunga jijini Dar es Salaam leo.
Wawakilishi
wa Kampuni ya Shamo World Foundation, Salama na Zaituni Ramadhani
wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wa kituo cha kulelea watoto
yatima na watoto walio klatika kituo hicho jijini Dar es Salaam leo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni