Jumanne, 12 Julai 2016

RAISI MAGUFULI AAGIZA VYOMBO VYA SERIKALI KUTUMIA MASHINE ZA EFD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli amewaagiza makatibu wakuu kuhakikisha vyombo vyote vinavyokusanya mapato serikalini vinatumia mashine za kielekrtoniki (EFD).
 
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi wateule wa Halmashauri,Wilaya,Majiji na Manispaa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi hao wa umma.
 
“Vyombo vya Serikali lazima vianze kutumia mashine za EFD,haiwezekani  wafanyabiashara wawe na mashine za EFD alafu maafisa wa serikali hawana,kama tumeamua kwenda kwa elektroniki lazima twende hivyo”Alisema Rais Magufuli.
 
Aidha amewataka wakurugenzi  wote kuchukua mashine hizi na kwenda nazo katika maeneo yao ya kazi ili ziwasaidie katika ukusanyaji wa mapato ya serikali katika halmshauri zao.
 
Hali kadhalika amewaagiza wakurugenzi hao kukusanya kodi na kutatua kero za wananchi wa chini zisizokuwa na lazima na kuongezea kuwa kama watakuta watendaji wa chini yao wasioendana  na kasi ya awamu ya tano basi watumie madaraka yao kuwaweka sawa.
  .
 
Aidha Rais magufuli amewataka wakurugenzi hao kusimamia kuanzishwa kwa viwanda vidogo vidogo katika maeneo yao ili kukamilisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni